• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yajibu kauli ya Marekani kuhusu waraka mweupe wa China

    (GMT+08:00) 2019-06-05 08:35:08

    Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Gao Feng amejibu taarifa ya Marekani kuhusu waraka mweupe uliotolewa hivi karibuni na China.

    Gao Feng amesema, Marekani imechukua hatua za upande mmoja na kujilinda, na kukiuka kanuni za biashara ya pande nyingi, na kuongeza kuwa, nchi hiyo pia imejaribu kuishawishi China kukubali masharti yake katika majadiliano ya kiuchumi na kibiashara. Amesema inadhihirika wazi ni nani amekiuka kanuni za kimataifa na ni nani anafanya vitendo visivyo na usawa vya kibiashara.

    Jumatatu wiki hii, Ofisi ya Ujumbe wa Biashara ya Marekani na Idara ya Hazina nchini humo zilitoa taarifa kuhusu waraka huo ulioitwa "Nafasi ya China katika Majadiliano ya Kiuchumi na Biashara na Marekani".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako