• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani zinazofanyika mjini Hangzhou

    (GMT+08:00) 2019-06-05 17:42:47

    Rais Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya mazingira duniani zinazofanyika mjini Hangzhou, hapa China, na kutoa mwito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja kuhimiza maendeleo yasiyo na uchafuzi, yenye utoaji mdogo wa hewa ya carbon na yaliyo endelevu.

    Kwenye barua yake, Rais Xi amesema, "Tuna dunia moja. Kulinda mazingira yake ya kuhimiza maendeleo endelevu ni jukumu letu la pamoja".

    Rais Xi pia amesema kutokana na jumuiya ya kimataifa kuhimiza kwa makini utekelezaji wa ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu kuelekea mwaka 2030, nchi mbalimbali zinakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa na kupungua kwa uanuai wa viumbe.

    Rais Xi pia amekumbusha kuwa China inazingatia umuhimu wa ulinzi wa mazingira, na kufanyia kazi uelewa kuwa maji safi na milima ya kijani ni mali muhimu, na kutafuta mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako