• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yatarajia kutumia maonesho ya biashara ya China na Afrika kuvutia uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:18:36

    Serikali ya Sudan Kusini na maofisa wa biashara wa nchi hiyo wanatarajiwa kushiriki kwenye maonesho ya uchumi na biashara ya China na Afrika yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, kuvutia uwekezaji nchini Sudan Kusini.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini Bw. Mawien Ariik amesema Sudan Kusini inafurahia kujiunga na nchi 52 za Afrika kushiriki kwenye maonesho hayo, yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 27 hadi tarehe 29 Juni, mkoani Hunan.

    Bw. Ariik amesema hii ni fursa nzuri kwa Sudan Kusini kwa sababu kutakuwa na jukwaa la kufahamisha kuwa Sudan Kusini inafanya bidii kufanikisha amani ya kudumu na ni salama kwa kufanya biashara.

    Kwenye maonesho hayo yanayotarajiwa kufanyika mjini Changsha, wageni 1500, wenyeji 5000, na wengine 3,500 watakaoonesha bidhaa, wateja na wanataaluma, watashiriki kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako