• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataka kesi ya kuhujumu uchumi kuharakishwa

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:25:02

    Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) Archard Kalugendo na wenzake umeutaka upande wa mashtaka wafanye jitihada za kukamilisha upelelezi.

    Wengine wanaoshtakiwa ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu ambaye ni afisa kutoka wizara ya madini

    Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa jalada lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na upelelezi upo kwenye hatua za mwisho hivyo mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

    Wakili wa utetezi Hassan Kiangio alidai shauri hilo lipo mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili hivyo upande wa mashtaka wafanye jitihada za kukamilisha upelelezi.

    Baada ya maelezo hayo, Hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Juni 14, 2019 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako