• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasiwasi watanda kwa wanaoficha fedha majumbani Kenya

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:25:25
    Wasiwasi bado umeendelea kuwakumba wafanyibiashara wenye mazoea ya kuficha pesa majumbani mwao siku chache tu baada ya serikali kutangaza noti mpya.

    Hii ni baada ya serikali kuchukua hatua ya kukabiliana na watu walioficha manyumbani mwao pesa wanazopata kupitia ufisadi na ulanguzi wa fedha kwa kufutilia mbali noti za Sh1,000 na kuanzisha noti mpya.

    Jumamosi, Gavana wa Benki Kuu ya Kenya, Patrick Njoroge alisema noti zote za Sh1,000 zilizokuwa zikitumika zinapaswa kubadilishwa na zile mpya kufikia Oktoba 1.

    Hii inamaanisha kwamba watakaokosa kubadilisha pesa hizo kufikia tarehe hiyo hawataweza kuzitumia mahali popote kwa sababu zitakuwa haramu.

    Dkt Njoroge alitoa tangazo hilo Rais Uhuru Kenyatta alipozindua noti mpya za sarafu mbalimbali punde tu baada ya kuongoza taifa kuadhimisha Siku ya 56 ya Madaraka katika Kaunti ya Narok.

    Kulingana na gavana huyo, noti za Sh1,000 zimekuwa zikitumiwa na watu laghai wanaotengeza pesa feki ambao huhofia kuzipeleka katika benki wakihofia kuchunguzwa na asasi husika za serikali. Kuficha pesa majumbani kadhalika hupunguza kusambaa kwa pesa miongoni mwa wananchi na hivyo kutatiza biashara, uwekezaji na hata ustawi wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako