• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CRDB yasema ukosefu wa vigezo ni kikwazo cha biashara kwa wanawake

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:25:42

    Ukosefu wa vigezo vya kupata mikopo umesababisha wanawake nchini Tanzania kushindwa kunufaika na fursa ya mkopo maalumu kwa wanawake unaotolewa na Benki ya CRDB.

    Meneja Biashara wa benki hiyo Mkoa wa Tanga, Benedicta Mshanga amesema benki hiyo imetoa fursa hiyo ya mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake lakini wameshindwa kuitumia fursa hiyo. Ameongeza kuwa wanawake wengi wameshindwa kunufaika na fursa hii ya mkopo kutokana na kukosa vigezo huku wengine biashara zao zikifa baada ya kupata mkopo biashara.

    Pamoja na mambo mengine, amesema lengo la benki hiyo ni kuhakikisha wanatoa kipaumbele maalumu cha kuhakikisha wanamuinua mwanamke wa Kitanzania ambapo amewashauri wanawake wajasiriamali kuhakikisha wanatumia fursa hiyo ya mikopo ili kuinua mitaji yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako