• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyeri kuunda kiwanda cha parachichi

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:26:00

    Gavana wa kaunti ya Nyeri nchini Kenya Bw Mutahi Kahiga amesema serikali ya kaunti ya hiyo inapania kuunda kiwanda cha maparachichi ili kupiga jeki ukuzaji wa zao hili.

    Amesema hatua hii pia inalenga kufanya maparachichi kuwa miongoni mwa mazao yanayoingizia wakulima mapato.

    Kahiga amesema mradi huu umepangiwa kugharimu kiasi cha Sh50 milioni.

    Kwa muda wa miaka miwili iliyopita, Serikali ya Kaunti ya Nyeri imeonekana kuwa katika mstari wa mbele kuhimiza wakulima kuvalia njuga ukuzaji wa matunda haya.

    Aidha, imekuwa ikisambaza miche kwa wakulima bila malipo sawa na kaunti ya Murang'a.

    Aprili 2019 Kenya ilitia saini mkataba wa kuuza maparachichi nchini China.

    Rais Uhuru Kenyatta alisema mpango huo utasaidia kuinua kilimo cha avocado hapa nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako