• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka Korea Kaskazini na Marekani kuhimiza mchakato wa utatuzi wa kisiasa wa suala la Peninsula ya Korea kupata maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:44:50

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inazitaka Korea Kaskazini na Marekani kufuatilia ufuatiliaji halali wa upande mwingine na kuhimiza mchakato wa utatuzi wa kisiasa wa suala la Peninsula ya Korea kupata maendeleo.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini amesema, mwaka jana Marekani ilikwepa kwa makusudi kutekeleza taarifa ya pamoja ya nchi hizo mbili iliyotolewa huko Singapore, na kuitaka Korea Kaskazini kuacha nyuklia kwa upande mmoja. Kama taarifa hiyo itakuwa karatasi tupu au la, itategemea jinsi Marekani itakavyojibu msimamo wa Korea Kaskazini.

    Bw. Geng amesema mwezi wa Juni mwaka jana viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani walifanya mkutano wa kihistoria na kutoa taarifa ya pamoja, suala la Peninsula ya Korea lilirudi tena katika njia sahihi ya mazungumzo. Hivi sasa mchakato wa mazungumzo ya suala hilo uko katika kipindi muhimu, hivyo China inazitaka pande hizo mbili kuendelea kutekeleza makubaliano, na itashirikiana na jumuiya ya kimataifa na kutoa mchango katika utatuzi wa suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako