• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vipindi kuhusu Nukuu za kifasihi anazopenda Rais Xi Jinping wa China vyatangazwa

    (GMT+08:00) 2019-06-05 19:54:18

    Wakati rais Xi Jinping wa China anafanya ziara rasmi nchini Russia, vipindi vya "Nukuu za kifasihi anazopenda rais Xi Jinping" toleo la lugha ya kirusi, vimeanza kutangazwa rasmi kuanzia leo tarehe 5 mjini Moscow. Idhaa ya habari ya Shirika la Radio na Televisheni la Russia na idhaa ya kirusi ya Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China zinatangaza kwa wakati mmoja vipindi hivyo.

    Vipindi hivi vilivyotengenezwa na Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China vimekusanya nukuu maarufu za kifasihi rais Xi Jinping wa China alizonukuu na kutumia kwenye hotuba na makala zake, ambavyo vimeonesha uelewa wa kina wa rais Xi kuhusu mila na desturi za China, na chanzo cha nadharia yake kuhusu utawala wa nchi.

    Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambaye pia ni mkuu wa Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China Bw. Shen Haixiong akihutubia sherehe ya uzinduzi amesema, vipindi hivyo si kama tu vitawafungulia warussia dirisha la kushuhudia wazo na uzuri wa rais Xi Jinping, bali pia vitatoa njia mpya ya kufahamu uzuri wa utamaduni wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako