• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • JUDO: Tanzania yapewa nafasi sita michezo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-06 08:09:55

    Timu ya taifa ya Judo ya Tanzania imepewa nafasi sita za kushiriki michezo ya Afrika (All African games) itakayofanyika mwezi Agosti nchini Mororcco.

    Katibu wa Judo, Innocent Malya amesema watafanya mchujo kwa wachezaji 12 wanaoendelea na kambi jijini Dar es Salaam. Amesema wamepatiwa nafasi hizo sita, lakini ni mapema sasa kuwataja wachezaji hao sita watakaowakilisha nchi hiyo kwenye michuano hiyo.

    Mbali na Judo, mchezo mwingine utakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ni Riadha, ambapo katibu mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania WilhelimGidabuday amebainisha kuwa watateua timu baada ya mashindano yatakayofanyika Arusha Julai 6 na 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako