• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapanga kuhimiza usafirishaji wa bidhaa kwa nje

    (GMT+08:00) 2019-06-06 08:51:04

    Kenya jana imelaani kuongezeka kwa pengo la biashara, na kuonya kuwa hali hiyo huenda itaathiri uendelezaji wa viwanda nchini humo.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa maonesho ya kimataifa ya nane ya biashara ya maua, Waziri wa viwanda, biashara na ushirika wa Kenya Bw. Chris Kiptoo amesema jijini Nairobi kuwa, hivi sasa thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya Kenya ni mara tatu kuliko mauzo ya bidhaa kwa nje. Amesema Kenya itaongeza usafirishaji wa bidhaa kwa nje kwa angalau asilimia 25 kila mwaka ili kupunguza nakisi kwenye urari wa biashara.

    Vilevile amesema Kenya inataka kutumia makubaliano ya biashara yaliyopo kati yake na nchi nyingine ili kuhimiza usafirishaji wa bidhaa kwa nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako