• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisi ya pamoja ya tahariri kati ya CMG na Gazeti la Russia la Rossiyskaya Gazeta yazinduliwa rasmi

    (GMT+08:00) 2019-06-06 08:51:16

    Ofisi ya pamoja ya tahariri kuhusu mambo ya China na Russia iliyoanzishwa chini ya ushirikiano kati ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Gazeti la Russia la Rossiyskaya Gazeta, imezinduliwa rasmi mjini Moscow.

    Naibu waziri wa Idara ya uenezi ya Kamati kuu ya chama cha kikoministi cha China na Mkurugenzi mkuu CMG Bw. Shen Haixiong na mkurugenzi mkuu wa Gazeti la Russia la Rossiyskaya Gazeta Bw. Pavel Negoitsa walihudhuria hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo.

    Akihutubia hafla hiyo, Bw. Pavel Negoitsa amesema kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni hatua mpya muhimu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na anatumai kuwa zitatumia vizuri nguvu zake bora na kukumbatia teknolojia mpya, ili kuinua ushirikiano kati yao ufikie ngazi mpya.

    Kwa upande wake, Bw. Shen Haixiong amesema kuzinduliwa kwa ofisi hiyo ya tahariri ni jaribio jipya la ushirikiano kati ya CMG na Rossiyskaya Gazeta unaolenga kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia, na kuongeza ushawishi wa vyombo vya habari vya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako