• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wiki ya biashara ya China yaanza nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-06-06 09:12:25

    Wiki ya tano ya Biashara ya China imeanza katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi hapo jana, ambapo zaidi ya washiriki 500 wataonyesha bidhaa zilizotengenezwa kwa ubora wa juu kutoka nchini China.

    Waziri wa Ugatuzi wa Kenya Eugene Wamalwa amefungua maonyesho hayo yanayotarajiwa kuvutia watu 30,000 wenye nia ya kununua bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo, vifaa vya kielektroniki, bidhaa za matumizi ya nyumbani na vipuri vya magari.

    Wamalwa amesema, Kenya ni nchi inayoibuka kiuchumi ambayo ina nia ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara wa pande mbili na China kupitia maonyesho na pia majukwaa ya kibiashara. Ameongeza kuwa, Wiki ya Biashara ya China inawakilisha jukwaa kwa Kenya na China kubadilishana uzoefu na maoni na hivyo kuboresha uhusiano mzuri wa kiuchumi kati ya nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako