• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Sudan yatangaza kuwa watu 46 wameuawa kwenye mapambano mjini Khartoum

    (GMT+08:00) 2019-06-06 18:39:39

    Serikali ya Sudan imetangaza kuwa watu 46 wameuawa wakati jeshi linawatawanya watu waliofanya maandamano ya kukaa kwenye mbele ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum. Naibu katibu mkuu wa wizara ya afya ya nchi hiyo Bw. Suleiman Abdul-Jabar amesema idadi ya watu waliouawa haijazidi 46, licha ya habari kutoka kwa wapinzani kusema watu zaidi ya 100 wameuawa.

    Habari pia zinasema mwenyekiti wa baraza la kijeshi la Sudan Bw. Abdel-Fattah Al-Burhan ameongea kwa njia ya televisheni akiwataka wapinzani kufanya mazungumzo na serikali kwa ajili ya maslahi ya taifa na kuepuka msukosuko. Hata hivyo makundi makubwa ya upinzani yamekataa mwito huo, na kumtaka mwenyekiti wa baraza la kijeshi ajiuzulu kutokana na kuwatawanya waandamanaji wanaokaa mbele ya makao makuu ya jeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako