• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya usimamizi wa mazingira ya Rwanda yasema kilimo kinachangia sana utoaji wa hewa chafu

    (GMT+08:00) 2019-06-06 18:45:23

    Idara ya usimamizi wa mazingira ya Rwanda (REMA) imetoa taarifa ikionesha kuwa sekta ya kilimo inachangia sana kwenye utoaji wa hewa chafu nchini humo.

    Ripoti kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ya idara hiyo, inaonyesha kuwa utoaji wa hewa chafu kutoka kwenye sekta hiyo unachukua asilimia 70.4 ya jumla ya kitaifa, hasa kwa sababu ya mbolea, katika mwaka 2015.

    Ripoti hiyo inaongeza kuwa Rwanda inahitaji kusimamia taka ngumu na maji ili kupunguza utoaji wa hewa chafu.

    Katibu wa wizara hiyo Bi. Fatina Mukarubibi amesema kudhibiti vyanzo vya utoaji wa hewa chafu, kunahitaji juhudi za pamoja za watu binafsi na serikali, ikiwa ni pamoja na sera, sheria, kanuni na vitendo ili kuboresha ubora wa hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako