• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki Kuu ya Kenya (CBK) yatoa sheria kali za ubadilishaji wa noti mpya

    (GMT+08:00) 2019-06-06 18:47:35
    Bila ya akaunti ya Benki,hautaweza kubadilisha zaidi ya Sh1 milioni ya sarafu za zamani ili kupata noti mpya nchini Kenya.

    Katika hatua nyengine ya kukinga mchakato wa kuondoa sarafu za zamani katika soko,Benki Kuu ya Kenya imeagiza benki za kibiashara kuomba idhini kwanza kabla ya kufanya muamala wa namna hiyo.

    Gavana wa Benki Kuu ya Kenya,Patrick Njoroge amesema mtu yeyote ambaye atakuwa na fedha zinazozidi Sh milioni 1 atahitajika kupata idhini kutoka CBK kabla ya kubadilisha fedha hizo na kupata noti mpya.

    Hii inamaanisha kwamba wakenya walio na kiasi kikubwa cha fedha watahitajika kufungua akaunti ya benki au kupoteza pesa zao.

    Kenya iko katika hatua za kuondoa sokoni sarafu za zamani na kuleta nyingine mpya,shughuli ambayo inatarajiwa kukamilika tarehe 1 Oktoba.

    Sekta ya sanaa na burudani nchini Tanzania imeongoza katika kuchangia pato la taifa kwa asilimia 13.6.

    Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema sekta hiyo na ile ya habari na mawasiliano zimeendelea kufanya vizuri na kukua wa kasi.

    Alisema sekta zilizokua kwa kasi kubwa ni pamoja na sanaa na burudani (asilimia 13.6),ujenzi (asilimia 12.9),usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8),na habari na mawasiliano (asilimia 9.1).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako