• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yatabiri ukuaji wa uchumi wa Uganda 2019

    (GMT+08:00) 2019-06-06 18:47:52

    Kiwango cha Ukuaji wa Pato la taifa la Uganda (GDP) kimebashiriwa kukua kutoka asilimia 6 katika mwaka wa fedha 2018/2019 hadi 6.5% katika mwaka wa fedha 2019/2020.

    Hayo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia.

    Kulingana na makala ya 13 ya Ripoti ya Uchumi wa Uganda ya Benki ya Dunia,uwekezaji wa umma na kibinafsi unatarajiwa kupiga jeki ukuaji huo.

    Ripoti hiyo inasema ukuaji huo utaimarishwa zaidi na uwekezaji katika sekta za nishati,hifadhi za viwanda,matayarisho kwa ajili ya uzalishaji mafuta,na upanuzi unaoendelea wa miundomsingi ya teknolojia ya habari.

    Kulingana na Ripoti hiyo,ukuaji wa uchumi unatarajiwa kushuka kiasi katika mwkaa wa fedha 2020/2021 kutokana na uchaguzi Mkuu,kwa sababu shughuli za kisiasa na wasiwasi huenda zikasababisha kushuka kwa uwekezaji na shughuli za kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako