• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yatoa Ripoti ya uchunguzi juu ya hali ya Marekani kunufaika kwenye ushirikiano kati yake na China

    (GMT+08:00) 2019-06-06 19:23:21

    Wizara ya biashara ya China leo imetoa Ripoti ya uchunguzi juu ya hali ya Marekani kunufaika na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya yake na China, ambayo inafafanua kuwa ushirikiano huo umeziletea nchi hizo mbili pamoja na wananchi wao faida halisi, Marekani inanufaika sana na ushirikiano huo.

    Ripoti hiyo inasema katika miaka 40 iliyopita tangu China na Marekani zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi mbili umepata maendeleo makubwa. Mwaka jana thamani ya biashara ya bidhaa kati ya nchi mbili imefikia dola bilioni 633.5 za kimarekani, thamani ya biashara ya huduma imefikia dola zaidi ya bilioni 125 za kimarekani, na thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa pande mbili imefikia takriban dola bilioni 160 za kimarekani.

    Ripoti hiyo inasisitiza kuwa urari mbaya wa biashara kati ya Marekani na China linatokana na sababu za kihistoria, hali ambayo inatokana na utendaji wa soko. Ingawa China ina urari mzuri wa biashara, pande zote mbili zinapata maslahi, na zinapaswa kudhamiria kuhimiza ushirikiano huo uwe wa kiwango cha juu na ubora zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako