• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafanya maonesho ya utalii kwenye nchi za Ulaya

    (GMT+08:00) 2019-06-07 08:14:08

    Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) imesema imezindua maonyesho ya utalii ya siku sita katika baadhi ya nchi za Ulaya kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini humo.

    Ofisa masoko wa Bodi hiyo Francis Malugu amesema, kampuni 10 za utalii kutoka Tanzania zinashiriki kwenye maonyesho hayo yaliyoanza Juni 3 na yanatarajiwa kumalizika Juni 8 katika miji ya London, Brussels, Paris na Lyon.

    Ujumbe wa Bodi hiyo umekutana na kampuni 135 za utalii katika miji hiyo, ambazo zimekubali kuanza kutangaza Tanzania kama kituo cha watalii katika nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako