• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika kumpa heshima rais wa zamani wa Zambia kutokana na mchango wake wa uhuru wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-07 08:14:27

    Umoja wa Afrika (AU) umesema utampa heshima ya kipekee aliyekuwa rais wa Zambia, Kenneth Kaunda kutokana na mchango wake katika kupigania uhuru wa Afrika.

    Mwezi uliopita, serikali ya Zambia ilieleza wasiwasi wake kuwa Kaunda ni rais pekee wa Afrika aliyepigania uhuru wa bara hilo, lakini hajapewa heshima yoyote na Umoja wa Afrika kupitia uwepo wa sanamu yake katika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Mousa Faki Mahamat amesema, nafasi ya rais Kaunda kamwe haijapingwa, na kwamba daima Afrika itamshukuru kwa mchango wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako