• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Gianni Infantino achaguliwa bila kupingwa kuendelea kuwa rais wa FIFA

    (GMT+08:00) 2019-06-07 08:28:06
    Gianni Infantino amechaguliwa kuongoza shirikisho la soka duniani FIFA, kwa muhula wa pili wa miaka minne, utakaokamilika mwaka 2023.

    Hatua hii imekuja baada ya kukosekana kwa mpinzani wa Infantino, wakati wa mkutano mkuu wa FIFA unaoendelea jijini Paris nchini Ufaransa.

    Infantino, mwenye umri wa miaka 49 raia wa Uswisi na Italia, alichaguliwa kuwa rais wa FIFA mwaka 2016 baada ya kuondoka kwa rais wa zamani Sepp Blatter.

    Baada ya kuchaguliwa tena, Infantino amesema kuwa, wakati wa miaka mitatu ambao amekuwa madarakani, taswira ya soka duniani imebadilika na kuwa na maendeleo makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako