• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamii ya Wachina nchini Namibia yachangia maendeleo ya elimu nchini humo

    (GMT+08:00) 2019-06-07 09:00:40

    Serikali ya Namibia imepokea vifaa halisi na samani katika Shule ya Mchanganyiko ya John Alphons Pandeni iliyoko mkoa wa Omusati vilivyotolewa na jamii ya wafanyabiashara wa China katika eneo hilo.

    Vifaa hivyo ni pamoja na samani, vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine zenye thamani ya dola za kimarekani 10,000 kwa ajili ya maendeleo ya shule hiyo.

    Kaimu mkurugenzi wa Elimu katika mkoa wa Omusati Bi. Sophia Ashipala amesema, mchango huo utasaidia kukabiliana na uhaba wa miundombinu ya elimu na vifaa vya kufundishia nchini Namibia.

    Mshauri wa kisiasa wa ubaliozi wa China nchini Namibia Yang Jun amesema, uwekezaji huo uliofanywa na jamii ya Wachina unalenga kuboresha upatikanaji wa elimu nchini Namibia, na pia unasaidia kukabiliana na changamoto ya kuwawezesha wanafunzi kupata elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako