• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa mpito wa Algeria atoa mwito wa mazungumzo ili kutatua mgogoro

    (GMT+08:00) 2019-06-07 09:38:36

    Rais wa mpito wa Algeria Abdelkader Bensalah amehimiza vyama vya kisiasa na wawakilishi wa mashirika ya kiraia kuanzisha mazungumzo kwa ajili ya kuitoa nchi hiyo kwenye mgogoro wa kisiasa ulioanza mwezi Februari.

    Wito huo umetolewa kufuatia baraza la kikatiba nchini Algeria kufuta uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Julai 4. Hii ni mara ya pili kwa rais Bensalah kuhimiza vyama vya kisiasa kuanza mazungumzo, miezi miwili baada ya mwito wake wa kwanza kususiwa na watu mashuhuri na vyama vya upinzani.

    Juni 2, Baraza la Kikatiba nchini humo liliamua kufuta uchaguzi mkuu baada ya kuthibitisha kuwa wagombea wawili waliowasilisha fomu za usajili walishindwa kutimiza masharti yanayotakiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako