Polisi wa Malawi wametumia gesi ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha upinzani cha MCP waliokuwa wakipinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 21. Msemaji wa polisi James Kadadzera amesema askari polisi walifanya hivyo bila kufahamu kuwa balozi wa Marekani nchini humo Virginia Palmer alikuwa kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho. Tarehe 27 mwezi uliopita, Tume ya uchaguzi ya Malawi ilitangaza rais Peter Mutharika ameshinda tena uchaguzi mkuu, matokeo yaliyosusiwa na wafuasi wa vyama vya upinzani, ambao wamefanya maandamano kwa njia ya amani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |