• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuboresha utendaji wake wa kazi

    (GMT+08:00) 2019-06-07 09:55:45

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, China inazingatia kuboresha utendaji kazi za Baraza la Usalama la Umoja huo ili kuongeza ufanisi na mamlaka yake.

    Bw. Wu amesema, Baraza hilo linalolenga kudumisha amani na usalama wa kimataifa, linapaswa kufuatilia zaidi masuala makubwa yanayotishia amani na usalama wa dunia na kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi fulani yasiyoathiri amani na usalama.

    Bw. Wu pia amependekeza Baraza hilo kutafuta mwafaka kupitia majadiliano ya kina, na kuzitaka nchi wajumbe wa Baraza hilo kuongeza mawasiliano na ushirikiano ili kuzingatia maoni ya pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako