• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yaonya kuwa mgogoro wa kibiashara utauletea uchumi wa Marekani hatari halisi

    (GMT+08:00) 2019-06-07 17:06:17

    Shirika la fedha la kimataifa IMF limeonya kuwa hali ya wasiwasi ya mgogoro wa kibiashara na mabadiliko ya mazingira ya soko la fedha, vitauletea uchumi wa Marekani hatari halisi.

    IMF imetabiri kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Marekani itapungua hadi asilimia 2.6 katika mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 2.9 ya mwaka jana, kiasi ambacho kitapungua hadi kufikia takriban asilimia 2 mwakani.

    Shirika hilo limeonya kuwa hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwenye sekta ya uagizaji kutoka nje na hatua zake nyingine zinaharibu mfumo wa kibiashara wa dunia, na kusababisha hatua za kibiashara za mfululizo dhidi ya vikiwazo vilivyowekwa na Marekani. Kama hali ya mgogoro wa kibiashara itazidi kuwa mbaya, au kama mazingira ya soko la fedha yatabadilika ghafla, uchumi wa Marekani utakabiliwa na hatari halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako