• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asema kupeana shahada ya heshima ya uzamivu kwa viongozi wa China na Russia ni ishara ya uhusiano wa kiwango cha juu kati ya nchi mbili

    (GMT+08:00) 2019-06-07 17:07:05

    Rais Xi Jinping wa China jana alihudhuria hafla ya kupewa shahada ya heshima ya uzamivu ya Chuo Kikuu cha St. Petersburg, mkuu wa chuo hicho Bw. Nikolai Kropachev amempa rais Xi cheti cha shahada hiyo.

    Kwenye hotuba yake, rais Xi amesema viongozi wa China na Russia kupeana shahada ya heshima ya uzamivu, ni mfano mzuri wa mawasiliano ya karibu kwenye sekta za elimu na utamaduni kati ya nchi mbili, pia ni ishara muhimu ya uhusiano wa kiwango cha juu kati ya China na Russia. Amezitaka pande zote mbili ziendelee kupanua mawasiliano na ushirikiano, kueneza utamaduni wa pande mbili, ili kuwaandaa wataalamu wengi zaidi kwa ajili ya maendeleo ya nchi hizo mbili.

    Mwezi Aprili mwaka huu, Chuo Kikuu cha Tsinghua cha China kilimpatia rais Vladimir Putin wa Russia shahada ya heshima ya uzamivu, na rais Xi alihudhuria hafla hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako