• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yatumai kuongeza uzalishaji wa kahawa ili kuongeza fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2019-06-07 17:12:16

    Uganda inatekeleza hatua za kuhimiza uzalishaji wa kahawa ili kuongeza mapato ya fedha za kigeni.

    Kwenye hotuba kwa taifa aliyoitoa jana kwenye bunge la Uganda, Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema serikali inaweka mkazo kwenye kusambaza mbegu bora, kuboresha kazi ya kuvuna, kazi baada ya kuvuna na utunzaji.

    Rais Museveni amesema kama Uganda inaweza kuongeza uzalishaji wa kahawa kwa hekta kuanzia tani 0.67za sasa na kufikia tani 2.2 kama Brazil na Vietnam, Uganda itakuwa inaingiza dola bilioni 2 za kimarekani kutokana na kahawa ghafi.

    Amesema kwa uzalishaji kama huo, Uganda itazalisha magunia milioni 21 ya kahawa kwa mwaka, na kama kahawa hiyo ikikaangwa kabla ya kuuzwa nje, inaweza kuingiza dola bilioni 6.7 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako