• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano na wasikilizaji wa vipindi vya "Nukuu za kifasihi anazozipenda Xi Jinping" wafanyika huko St Petersburg

    (GMT+08:00) 2019-06-07 18:10:56

     

     

     

    Mkutano na wasikilizaji wa vipindi vya "Nukuu za kifasihi anazozipenda Xi Jinping" umefanyika jana kwenye Redio Metro mjini St. Petersburg, ambapo mkuu wa Kituo kikuu cha redio na televisheni cha China Bw. Shen Haixiong, mshauri wa uchumi wa rais wa Russia Bw. Sergey Glaziev, mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kimataifa ya shirika la habari la Sputnik nchini Russia Bw. Vasily Pushkov, na wajumbe zaidi ya 100 kutoka sekta za serikali, viwanda na biashara, na vyombo vya habari za Moscow na St. Petersburg wameshiriki kwenye shughuli hizo za mawasiliano.

    Bw. Shen amesema, baada ya kutangazwa nchini Russia, vipindi vya "Nukuu za kifasihi anazozipenda Xi Jinping" toleo la Kirusi vimekaribishwa na wasikilizaji wengi nchini humo, na hii imeonesha kuwa mustakabali wa ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya nchi hizo mbili ni mzuri sana.

    Bw. Sergey Glaziev amesema miradi ya mawasiliano ya utamaduni kati ya Russia na China ikiwemo "Nukuu za kifasihi anazozipenda Xi Jinping" imewavutia raia wengi wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako