• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wafanyabishara Gulu walalamikia uhaba wa wateja

    (GMT+08:00) 2019-06-07 19:47:17
    Wafanyabiashara wamehama kutoka soko kuu la Gulu wakilalamikia kupungua kwa biashara.

    Soko hilo lilijengwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 28 lakini wafanyabiashara wanasema ni vigumu kwa wateja kufika eneo hilo.

    Sasa wengi wa wafanya biashara hao wamepiga kambi nje ya soko hilo ambako kunaegeshwa magari.

    Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Gulu, Patrick Omaya, hata hivyo amesema wachuuzi waliokosa nafasi ndani ya soko ndio waliopiga kambi nje.

    Naye meya wa manispaa ya Gulu George Labeja, amesema wanachukua hatua za kusuluhisha tatizo lililopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako