• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia: Fujian Haian Rubber yafungua ofisi Zambia

    (GMT+08:00) 2019-06-07 19:47:52
    Kampuni ya kutengeneza matairi ya magari kutoka china imefungua ofisi nchini Zambia ikilenga kuuza bidhaa hizo kwenye soko la Afrika.

    Kampuni hiyo ya Fujian Haian Rubber kwa sasa inauza bidhaa zake katika kwa sekta ya uchimbaji nchini Zambia, DR Congo (DRC) Afrika Kusini na Senegal.

    Mkurungezi wa kampuni hiyo kanda ya Afrika Eric Lin, amesema kufunguliwa kwa makao makuu nchini Zambia ni mpango wa kufikia nchi nyingi barani humo.

    Alisema Zambia, imeendelea kuwa na utulivu wa kisiasa na hivyo kuwa na fursa nyingi za uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako