• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda cha kutengeneza taa kufunguliwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-06-07 19:48:09
    Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kwa kushirikiana na kampuni ya Everlight Skyzone ya China wanatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza taa za barabarani chenye thamani ya Sh. bilioni 12 za kitanzania.

    Lengo kuu la mradi huo ni kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuiingiza Tanzania katika uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

    Akizungumza na Nipashe, msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Kapteni James Mhame, alisema kiwanda hicho kitajengwa jijini Dar es Salaam eneo la Mlalakuwa ambalo ni Makao Makuu ya JKT na kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 50.

    Alisema ujenzi wa kiwanda hicho ulianza Aprili mwaka huu na unatarajia kumalizika Agosti mwaka huu.

    Kujengwa kwa kiwanda hicho kutaongeza fursa ya ajira kwa Watanzania na kuifanya nchi kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye viwanda vya taa za kisasa (LED) ambayo ni teknolojia mpya barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako