• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Russia yaitaka Uganda kuongeza mauzo yake Moscow

    (GMT+08:00) 2019-06-07 19:48:25
    Russia imeitaka Uganda kujinufaisha na fursa ya soko la dola bilioni 28 la vyakula.

    Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Uganda- Moscow mkurugenzi wa chama cha wafanyabiashara wa Russia Alexander V Kopkov, alisema kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kinafikia dola milioni 74 lakini asilimia 86 ni mauzo ya Russia kwenda Uganda.

    Uganda inauza nchini Russia bidhaa kama vile chai, kahawa na viungo na kuagiza dawa, chuma, vipuli na ngano kutoka Russia.

    Naye balozi balozi wa Uganda nchini Russia Johnson Olwa Agara, amesema serikali inapanga kuongeza mauzo kwenda Moscow hasa bidhaa za kilimo kama matunda na mboga na pia kuweka mipango wa kuvutia watalii zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako