Akitoa agizo hilo mjini Musoma kwenye mafunzo ya wajasiriamali wadogo wanaosindika vyakula, Kaimu Meneja TFDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Nuru Mwasulama, alisema ni vyema wazalishaji wa vyakula vya aina hiyo kufikisha elimu waliyopewa kwa wafanyakazi wao wanaosaidia kutengeneza vyakula hivyo.
Alisema iwapo mfanyakazi atagundulika kuwa na maradhi yaliyotajwa hataruhusiwa kufanya kazi kiwandani mpaka atakapopona.
Kadhalika alisema kiwanda kinatakiwa kuwa na sehemu maalumu zenye nafasi za kutosha kubadilisha nguo, maliwato na bafu ikiwamo sehemu ya kunawa mikono, na kwamba vyote vinatakiwa kukidhi mahitaji ya jinsia zote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |