• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China chafanya shughuli mbalimbali katika baraza la uchumi mjini St. Petersburg

    (GMT+08:00) 2019-06-07 20:07:26
    Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China na Mfuko wa Roscongress wa Russia leo wamesaini makubaliano kuhusu ushirikiano wa kimkakati, na kuzindua video kuhusu Miji rafiki kati ya China na Russia. Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Xiaohui, mkuu wa Kituo kikuu cha Radio na Televisheni cha China Bw. Shen Haixiong, naibu waziri wa maendeleo ya dijitali, mawasiliano na vyombo vya habari wa Russia Bw. Volin Aleksey Konstantinovich, pamoja na wajumbe kutoka ubalozi wa China nchini Russia na vyombo vya habari vya nchi hizo mbili wameshiriki kwenye shughuli hizo.

    Kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa, pande hizo mbili zitaimarisha ushirikiano katika sekta ya habari kwa kufuata kanuni za usawa, kunufaishana na wazi, chini ya mfumo wa baraza la uchumi la St. Petersburg na baraza la uchumi wa mashariki, ili kutoa habari nyingi zaidi zitakazoonesha ukweli wa mambo kwa watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako