• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNEP yashirikiana na Shirika la Maskauti kupamabana na uchafuzi wa plastiki

    (GMT+08:00) 2019-06-08 17:27:18

    Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na Shrika la Maskauti Duniani jana yalianzisha ushirikiano wenye lengo la kuanzisha harakati za kuchukua hatua kwenye mapambano dhidi ya uchafuzi wa palastiki.

    Mkurugenzi wa mfumo wa ikolojia wa UNEP Susan Gardner amesema mjini Nairobi kuwa ushirikiano huo unalenga kufanya kazi pamoja ili kuanzisha harakati mpya kwa vijana za kuchukua hatua duniani. Hadi sasa vijana 27,000 wa skauti, Shirika la Mwongozo wa wasichana (Girl Guide), Shirika la Junior Achievement na vyuo vikuu mbalimbali, wamechukua Beji za Changamoto mpya ya Plastiki ya Tide Turners tangu kuanzishwa nchini Ghana, Kenya, Uganda, Mauritius na Tanzania. Nchini Kenya Shirika la Mwongozo wa wasichana la Alice Moraa limewafunza zaidi ya vijana 5,000 kubadili tabia zao juu ya plastiki na linashughulikia kutekeleza mifumo sahihi ya kutupa taka katika kaunti ya Kisii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako