• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Mnangagwa asema Zimbabwe haiwezi kujiendeleza bila ya sarafu yake

    (GMT+08:00) 2019-06-08 17:48:25

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema nchi yake haiwezi kujiendeleza kama itazidi kutumia sarafu za nchi nyingine.

    Amesisitiza kuwa nchi yake inalenga kuanzisha sarafu yake muda utakapokuwa muafaka. Pia amesema serikali yake imepitisha sera ambazo zitapelekea kuanzishwa tena kwa sarafu yake ikiwa ndio njia pekee kwa nchi hiyo kuendelea. Zimbabwe iliacha kutumia sarafu yake mwaka 2009 baada ya kutokuwa na thamani kutokana na muongo mzima wa mfumuko mkubwa wa bei, na kuanza kutumia sarafu za mataifa mbalimbali.

    Rais Mnangagwa amesisitiza kuwa utawala wa sarafu nyingi umekuwa ukitumika ili kukabiliana na mfumuko huo uliokithiri mwaka 2008 na 2009 lakini haupaswi kuendelezwa katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako