• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaandaa shughuli mbalimbali za siku ya utamaduni na urithi

    (GMT+08:00) 2019-06-09 17:51:39

    Zaidi ya shughuli 3200 zimefanyika katika sehemu mbalimbali za China kuadhimisha siku ya utamaduni na urithi wa asili, ambayo huangukia jumapili ya pili ya kila mwezi juni.

    Shughuli mbalimbali pia zimefanyika kwenye mji wa Yan'an, mkoani Shaanxi ambako yalikuwa makao makuu ya shughuli za mapinduzi za chama cha kikomunisti cha China.

    Shughuli nyingine zimefanyika katika miji mbalimbali ya China kueleza umuhimu wa mafanikio yaliyopatikana kwenye utunzaji wa vitu vya kumbukumbu za utamaduni kwenye maeneo muhimu 4,296 ya ulinzi wa vitu vya kale na majumba ya makumbusho 5,354.

    Ijumaa iliyopita ilikuwa ni sikukuu ya jadi ya China ya mbio za mashua za dragon, ambayo huadihimishwa kumkumbuka mshairi wa kale wa China Qu Yuan, katika kaunti ya Zigui mkoani Hubei, ambako yalikuwa maskani ya mshairi huyo, shughuli mbalimbali zenye kauli mbiu ya utamaduni na urithi wa asili zilifanyika, ikiwa ni pamoja na mbio za mashua za dragon.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako