• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Afrika Kusini watakiwa kutoa ulinzi kwa mfanyakazi wa SABC

    (GMT+08:00) 2019-06-10 08:44:44

    Upande wa upinzani nchini Afrika Kusini umelitaka jeshi la polisi kutoa ulinzi kwa mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) Bw. Thami Zikode ambaye alipona kwenye jaribio la kumuua.

    Kauli hiyo imetolewa jana baada ya Bw. Zikode ambaye ni mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani wa Shirika hilo, kupona baada ya watu wasiojulikana kumshambulia kwa risasi nje ya nyumba yake mjini Johannesburg ijumaa jioni.

    Muungano wa upinzani wa Democratic Alliance (DA) umedai kuwa shambulizi hilo ni mpango ulioratibiwa katika juhudi za mtandao wa ufisadi ulioligeuza SABC kuwa mali yao na sasa wanakabiliwa na uwezekano wa kufichuliwa.

    Polisi wanamshikilia mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusika na shambulizi hilo na wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine watatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako