• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kuzidisha ushirikiano halisi na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati

    (GMT+08:00) 2019-06-10 08:52:00

    Naibu waziri mkuu wa China Bw. Hu Chunhua amesema China inapenda kupanua na kuimarisha ushirikiano halisi na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati (CEECs).

    Bw. Hu amesema hayo alipohutubia Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati uliofanyika mjini Ningbo, mashariki mwa China.

    Akipongeza mafanyikio yaliyopatikana katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili, Bw. Hu amesema China iko tayari kushirikiana na nchi za Ulaya Mashariki na Kati katika kuunganisha mikakati na mipango yao ya maendeleo, kupanua biashara, kuhimiza uwekezaji, na kuharakisha muunganiko wa miundombinu, ili kuendelea kupanua na kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kati ya pande hizo mbili.

    Kabla ya kuhudhuria mkutano huo, Bw. Hu alitembelea maonesho ya kwanza ya China na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati, na kukutana na wageni kutoka nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako