• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapambano mjini Tripoli yaaathiri elimu kwa wanafunzi 120,000

    (GMT+08:00) 2019-06-10 09:05:07

    Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) jana limesema, elimu ya wanafunzi karibu 120,000 katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, imeathiriwa kutokana na mapambano ya kutumia silaha.

    Taarifa iliyotolewa jana na UNICEF imesema, wakati mapambano mjini Tripoli yanapoingia mwezi wa tatu, hali ya wanafunzi shuleni imekuwa ngumu zaidi kwani wanahangaika kuendelea na elimu na masomo.

    Taarifa imesema, mwezi Aprili wizara ya elilmu ya Libya iliomba kufunga shule kwenye maeneo ya mapambano, hivyo kuathiri moja kwa moja elimu kwa wanafunzi hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako