• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kombe la Kagame: Baada ya Simba ya Tanzania kujiondoa, sasa Yanga nao watangaza kutoshiriki

    (GMT+08:00) 2019-06-10 09:14:09
    Baada ya wiki iliyopita kutolewa taarifa na klabu ya Simba ya Tanzania kutoshiriki michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai nchini Rwanda, Yanga nao wametoa taarifa ya kutoshiriki michuano hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga ya Tanzania, imeeleza sababu nne za kujitoa kwenye michuano hiyo ikiwemo wachezaji kumaliza mikataba yao na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu za usajili wa wachezaji wapya.

    Sababu nyingine ni kocha wao Mwinyi Zahera raia wa DRC na baadhi ya wachezaji wao kwenda kushiriki michuano ya AFCON nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako