• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AMISOM yadhamiria kuendeleza juhudi za amani Somalia

    (GMT+08:00) 2019-06-10 09:35:20

    Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kimeahidi kuendeleza juhudi za kurejesha utulivu nchini Somalia, ili kusaidia ujenzi wa miradi muhimu na miundombinu katika jamii mbalimbali nchini humo.

    Mjumbe maalumu wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya Somalia ambaye pia ni kiongozi wa AMISOM Bw. Francisco Madeira amesema, tume hiyo imetekeleza miradi 47 nchini Somalia mwaka jana, ikiwa ni pamoja na kujenga upya miundombinu iliyopo kama vile shule, visima vya maji, barabara na vituo vya afya. Pia amesema, tume hiyo pia imewapatia vijana, wanawake na familia zinazoongozwa na watoto fursa za kujiajiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako