• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 25 wauawa katika shambulizi jipya nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2019-06-10 09:35:40

    Polisi nchini Nigeria imesema watu 25 wameuawa jana kwenye shambulizi lililofanywa na kundi la watu waliokuwa na silaha mkoani Sokoto, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, huku washambuliaji wanne wakikamatwa akiwemo mwanamke mmoja.

    Kamishna wa polisi wa jimbo hilo Bw. Ibrahim Kaoje amesema shambulizi hilo lililotokea jumamosi usiku limeathiri vibaya vijiji vitatu vya Kalhu, Tsage na Geeri vilivyoko kwenye eneo la Rabah, kaskazini mwa Nigeria. Washambulizi hao pia wameiba ng'ombe, mbuzi, na vitu kadhaa vya thamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako