• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Akiba ya fedha za kigeni ya China yaongezeka dola za kimarekani bilioni 6.1 ifikapo mwishoni mwa Mei

    (GMT+08:00) 2019-06-10 19:29:54

    Takwimu zilizotolewa na mamlaka ya usimamizi wa fedha za kigeni ya China zimeonyesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, akiba ya fedha za kigeni ya China imefikia dola za kimarekani trilioni 3.101, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2, sawa na dola za kimarekani bilioni 6.1 kuliko mwishoni mwa mwezi Aprili.

    Msemaji wa mamlaka hiyo Bibi Wang Chunying, amesema mwezi Mei migongano ya kibiashara duniani ilipanda, sintofahamu ya Brexit na sababu nyingine ziliongeza hali ya kuepuka hatari kwenye soko, kiwango cha thamani ya dola la za kimarekani na kiwango cha dhamana duniani pia vimeongezeka.

    Bibi Wang Chunying amesema, katika mwaka huu hali ya uchumi wa China imeendelezwa kwa utulivu, hali ya mahitaji na utoaji kwenye soko la fedha za kigeni la China vina uwiano. Hali ya jumla ya uchumi wa China ni nzuri, na imetoa uungaji mkono wa kutosha kwa uendeshaji tulivu wa soko la fedha za kigeni, na kuweka msingi imara kwa utulivu wa akiba ya fedha za kigeni ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako