• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa waratibu wa utekelezaji wa matokeo ya FOCAC kufanyika

    (GMT+08:00) 2019-06-10 19:56:46

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, mkutano wa waratibu wa utekelezaji wa matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utafanyika tarehe 24 na 25 hapa Beijing. Maofisa wa China na nchi 54 za Afrika watahudhuria mkutano huo.

    Bw. Geng Shuang amesema baada ya mkutano wa kilele wa Beijing, China na Afrika zimeshirikiana kwa karibu, kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano huo na kupata maendeleo makubwa. Kutokana na hali ya kimataifa kubadilikabadilika kwa sasa, pande mbili zinaona kuna mahitaji ya kufanya mkutano wa waratibu, ambao utajadili utekelezaji wa matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing, kuongeza ushirikiano kati ya China na Afrika kuendelezwa kwa sifa bora na maendeleo endelevu, kuhimiza matokeo ya mkutano huo kunufaisha zaidi watu wa China na Afrika, na kuonyesha nia thabiti ya pande mbili kuimarisha ushirikiano, kushikilia hali ya pande nyingi, na kuhimiza kujenga jumuiya ya mustakabali wa pamoja ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako