• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara ya nje ya China yakua kwa asilimia 4.1 katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-06-10 19:58:44

    Takwimu kutoka ofisi kuu ya forodha ya China zinaonesha kuwa katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, biashara ya bidhaa ya nje ya China ilikua kwa asilimia 4.1 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na thamani yake kufikia dola za kimarekani trilioni 1.76.

    Bidhaa zilizouzwa nje zimeongezeka kwa asilimia 6.1 na thamani yake kufikia yuan trilioni 2.56, na bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ziliongezeka kwa asilimia 1.8 na thamani yake ilikuwa yuan trilioni 5.6. Katika kipindi hicho urari mzuri wa biashara pia uliongezeka kwa asilimia 45 na kufikia yuan bilioni 893.

    Katika kipindi hicho washirika wakubwa wa biashara wa China wamekuwa Umoja wa Ulaya, ukifuatiwa na nchi za ASEAN. Biashara na nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" pia iliongezeka kwa asilimia 9, na thamani yake kufikia yuan bilioni 3.49. Na bidhaa zilizouzwa zaidi ni za mashine na vifaa vya umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako