• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Hazard aweka rekodi Real Madrid

    (GMT+08:00) 2019-06-11 08:34:12
    Eden Hazard ameweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Real Madrid baada ya kusaini kujiunga na timu hiyo wiki iliyopita.

    Madrid walitoa taarifa rasmi mwishoni mwa wikiendi ikieleza wamemalizana na Hazard na kuwa atajiunga na klabu hiyo msimu ujao.

    Klabu hiyo imemvuta winga huyo aliyekuwa akikipiga Chelsea kwa ada ya pauni milioni 150 ambayo inamfanya kuwa mchezaji wa bei mbaya zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo.

    Ada ya Hzard imemfanya ampiku Gareth Bale kama mchezaji ghali zaidi ndani ya Real Madrid, ambaye alinunuliwa kwa pauni milioni 88.8

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako