• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM waahidi kuunga mkono nchi wanachama kuhimiza matumizi ya magari ya umeme

    (GMT+08:00) 2019-06-11 08:47:10

    Umoja wa Mataifa umeahidi kuunga mkono nchi wanachama kukumbatia miradi ya magari ya umeme.

    Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kanda ya Afrika Bibi Juliette Biao Koudenoukpo amesema Shirika hilo litaunga mkono nchi wanachama katika kuendeleza sera na kubadilishana uzoefu.

    Akiongea kwenye mkutano kuhusu kusawazisha vigezo vya utoaji wa hewa ya ukaa kwenye magari na wajumbe wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Bibi Koudenoukpo amesema Umoja wa Mataifa unachukua hatua hiyo kutokana na kuwa usafiri endelevu unatoa fursa za maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira, ikiwemo afya bora, ajira, uwekezaji, ushirikishi wa jamii na maisha bora ya watu.

    Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, uchafuzi wa hewa unasababisha vifo vya watu milioni 7 duniani kila mwaka, na watu laki sita kati yao wanatoka Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako