• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yatoa fursa bora zaidi kwa wafanyabiashara wa kigeni

    (GMT+08:00) 2019-06-11 09:13:34

    Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Miundombinu na Nishati Bw. Amani Abou-Zeid amesema, Afrika inatoa fursa bora zaidi kwa wenzi na wafanyabiashara wa kimataifa.

    Abou-Zeid amesema hayo katika majadiliano ya Afrika na Russia yaliyofanyika hivi karibuni kando ya Mkutano wa Baraza la Uchumi la Kimataifa la St. Petersburg. Amesema Afrika inatoa fursa hizo katika maeneo ya miundombinu ya kikanda, nishati, teknolojia ya kidijitali, kilimo, elimu, na sayansi na teknolojia.

    Pia amesisitiza zaidi kuwa, mafungamano ya bara la Afrika yanatokea wakati bara hilo linaungana zaidi na kuzungumza kwa sauti moja kuhusu masuala muhimu ya kimataifa, jambo linalotoa fursa kwa wawekezaji na wenzi wa kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako